Tanzania

English French German Italian Portuguese Russian Spanish

Figo ya nguruwe iliyopandikizwa kwa binadamu mgonjwa yafanya kazi

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 15:07
Mafanikio ya majaribio hayo yamesifiwa na madaktari waliofanya upasuaji huo kuwa ni "uwezekano wa miujiza".
Categories: Tanzania

Kimeta yadaiwa kuua wawili, 30 walazwa Kilimanjaro

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 14:56
Watu wawili wakazi wa wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamefariki dunia baada ya kula nyama ya ng'ombe anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa kimeta huku wengine zaidi ya watu 30, wakilazwa hospitalini.
Categories: Tanzania

Wawili wafungwa jela maisha kwa kubaka, kulawiti watoto

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 14:35
Mahakama ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro imewahukumu watu wawili kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka mitatu na kulawiti mwingine wa miaka tisa.
Categories: Tanzania

Facebook kuanza kulipa vyombo vya habari

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 13:11
Facebook imesema leo kuwa imefikia makubaliano na baadhi ya magazeti ya Ufaransa kuwa itaanza kulipia habari zao zinazowekwa katika tovuti zao na ambazo watumiaji watashirikisha wengine (share), ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Google kutangaza kuwa italipia habari zilizo kwenye tovuti kila zitakapotafutwa (search).
Categories: Tanzania

Gaddafi aandaa vikosi vya siri akiwa shuleni

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 13:04
Katika toleo lililopita tuliona jinsi kizazi kipya cha wanasiasa wa Libya kilivyoathiriwa na vuguvugu la mageuzi katika ulimwengu wa Waarabu, hususan baada ya mapinduzi yaliyofanywa na Gamal Abdel Nasser nchini Misri kwa kumpindua Mfalme Farouk I Julai 23, 1952 na yale yaliyofanywa na Abdul Karim Kassem wa Iraq kwa kumpindua Mfalme Faisal II wa Iraq katika mapinduzi ya Julai 14, 1958.
Categories: Tanzania

Mwenyekiti jela kwa kulisha mifugo mashamba ya wakulima

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 12:35
Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Morogoro, Lucas Lemomo, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kuingiza mifugo kwenye mashamba na kuharibu mazao ya wakulima.
Categories: Tanzania

Uchaguzi Konde ulivyoonyesha ukomavu wa demokrasia Zanzibar

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 12:10
Licha ya mivutano ya mara kwa mara ya kisiasa visiwani Zanzibar bado visiwa hivyo vimeendelea kuonyesha ukomavu wa kidemokrasia kila zinapofanyika chaguzi.
Categories: Tanzania

Serikali kutenga bajeti ya Kilimo hai 2022

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 11:52
Serikali ya Tanzania na Mapinduzi Zanzibar, zimeazimia kutenga bajeti kwa ajili ya kuendeleza kilimo hai nchini.
Categories: Tanzania

Sabaya, wenzake wawasilisha kusudio la kukata rufaa

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 10:27
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamewasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Alhamisi Oktoba 21, 2021 ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Oktoba 15.
Categories: Tanzania

TTCL yaelemewa deni la Sh403 bilioni

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 09:16
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limelemewa na deni la Sh403 bilioni ilhali mtaji ilionao ni wa Sh243.
Categories: Tanzania

Uhaba wa wahadhiri vyuo vikuu washtua

Mwananchi - Thu, 21/10/2021 - 08:18
Vyuo vikuu vya ndani vinakabiliwa na upungufu wa wahadhiri wenye sifa, kwa mujibu wa wakuu wa vyuo.
Categories: Tanzania

Kubwata bila data si ni kudata kabisa?

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 19:55
Unajua Makengeza, hapo zamani za kijikale, katika kukumbuka miaka kumi ya Mkataba wa Haki za Watoto, waheshimiwa wetu wa sponji wa mji unaodidimia waliamua kuwa na kikao maalumu kuhusu hali ya watoto nchini kwetu.
Categories: Tanzania

Vyama vya siasa, Msajili kazi nzito

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 19:52
Mkutano wa kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na wadau wa siasa nchini uliopangwa kufanyika kesho, umeahirishwa kwa kile kinachodaiwa ni kutoa nafasi kwa wadau wengi zaidi kushiriki kikamilifu.
Categories: Tanzania

Dk Mwinyi ateua vigogo akiwamo Kaimu Jaji Mkuu

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 18:59
Rais wa Zanzibar na Mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa nyadhifa mbalimbali akiwemo Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Categories: Tanzania

RC Mtaka azuia Sh47 milioni ziara ya madiwani

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 17:18
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amekataa kuidhinisha ombi la Sh47 milioni kwa ajili ya ziara ya Madiwani wa jiji hilo, akidai kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.
Categories: Tanzania

RC Tabora apigia debe muhogo unaoongeza nguvu za kiume

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 16:38
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian amesifia aina mpya ya muhogo ijulikanayo kama Tumbi Tari 4 akisema inaongeza nguvu za kiume.
Categories: Tanzania

Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mkewe apate utajiri

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 14:44
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemhukumu mkazi wa Kata Mjele, Wilaya ya Mbeya, Mateso Wilson (34) kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua na kunyofoa viungo vya mkewe.
Categories: Tanzania

Mahakama yapokea kumbukumbu za simu kesi ya Sabaya

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 13:53
Mahakama imetupilia mbali pingamizi la kutaka nyaraka mbalimbali zikiwemo kumbukumbu za kupiga na kupokea simu, kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa simu za aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake, zisipokelewe kama kielelezo katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Categories: Tanzania

Sababu za Jaji Siyani kujitoa kusikiliza kesi ya Mbowe na wezanke

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 13:09
Jaji Kiongozi, Mustapha Siyani amejitoa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Categories: Tanzania

Kigogo wa Vodacom apanda kizimbani kutoa ushahidi kesi ya Sabaya

Mwananchi - Wed, 20/10/2021 - 11:59
Meneja wa ulinzi na mshirika katika vyombo vya ulinzi na usalama Vodacom PLC makao makuu, James Wawenje emepanda kizimbani leo kutoa ushahidi katika kesi ya uhuumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita.
Categories: Tanzania